Wadudu na Magonjwa ya Kabeji
Wadudu
Viwavi weusi aina ya Cutworms
Hawa ni viwavi weusi wanapatikana kawaida katika hatua za mwanzo za ukuaji wa mmea. Hukata mashina usawa wa ardhi kusababusha mmea kuanguka. Nyunyizia mmea kwa UMEME baada ya kupandikiza kudhibiti cutworms.
Kidukari
Kidukari ni mdudu mdogo wa kijani au njano anaepatikana kwenye majani ya mboga mboga. Wananyonya utomvu kutoka kwenye mmea na pia wanabeba magonjwa.
Nzi weupe
Hawa ni wadudu wadogo weupe wanaopatikana chini ya jani.Wananyonya utomvu kutoka kwenye mmea
Sawflies na Black diamond moths
Ni kipepeo weusi wa kufifia – kijani kwa rangi na hatua yake ya buu au kiluilui ni mharibifu sana.
Wanakula majani kusababisha kupukutika. Kama hawajadhibitiwa, wanasababisha hasara ya 100% ya mazao. Nyunyizia kwa CYCLONE unapoona dalili ya kwanza ya kushambulia.
Magonjwa
Black rot
Ni bacteria kwenye udongo ambaye anaweza kusababisha hasara kabisa ya mazao kama hautadhibitiwa. Ni kawaida wakati joto ni jingi na udongo una unyevu. Dalili ni pamoja na ncha makavu ya njano au kahawia mikavu katika hatua za mwanzo za kushambulia. Baadaye, vichwa hegeuka vyeusi,laini na huanza kuoza na kutoa harusu mbaya. Kumudu, toa na haribu mabaki ya mazao yaliathirika, tumia miche misafi na yenye afya na aina inayohimili. Nyunyizia Sulcop DF kutoka Osho Chemicals, mapema na kisha rudia kila siku 10.
Madoa au Leaf Spot
Madoa Pia ni kuvu atokanaye na
udongo ambao ni kawaida kwenye hali unyevunyevu Husambazwa na kupepo,maji au vifaa vilivyoathirika. Dalili
ni pamoja na madoa ya kahawia na mwisho kufanya mashimo na majani
hukauka.Kudhibiti,panda mbegu zilizoidhinishwa na badili mazao. Nyunyiza
Sulcop, Control 70DF au Enrich kutoka Osho Chemicals.
Kuvu wa duara (Ringspot)
Ni
kuvu anaebebwa na upepo,mbolea ya samadi au mabaki ya mazao yaliyoathika.dalili
ni duara- kama doa la kahawia kijivu kwenye majani.Kudhibiti,panda mbegu
zilizoidhinishwa/miche yenye afya,badili mazao kwenye shamba lako.Nyuniza
Sulcop au Enrich kutoka Osho Chemicals.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Kabeji
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure