Kupandikiza Nyanya
Hatua 1
Pandikiza miche baada ya wiki 3-4( urefu wa 15 -25cm ama miche ikiwa na majani 3 -5)
Hatua 2
Wiki moja kabla ya kuhamisha, punguzia mimea maji li kuimarihsa mimea na kuwa ngumu
Hatua 3
Chimba mashimo futi 1 ½ kiumbali katika mshororo na mishororo ya futi 2 katiyazo na chenye kina cha ½ futi (15cm) kiurefu.
Hatua 4
Weka kiganja cha samadi na kifuniko cha mbolea ya kupandia kama Mavuno Planting NPK 10.26.10 kwa kila shimo.
Hatua 5
Changanya udongo, mbolea na samadi vyema.
Hatua 6
Ng’oa miche na udongo kiasi kwenye mizizi na ipande kisha imarisha udongo kuizunguka.
Hatua 7
Totesha tena na PEARL na CONTROL 70DF kutoka Osho Chemicals na mwagilia miche maji mara kwa mara.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Nyanya
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure