Usimamizi

Hatua 1: Nafasi
Wiki 2 baada ya kupandikiza,panda miche mipya ili kuchukuwa nafasi ya miche ambayo haikuota
Hatua 2: Utoaji kwekwe/nyasi
Palilia kila wiki 3-4 kuzuia wadudu, magonjwa na kuzuia ushindani kwa ajili ya virutubisho.
Hatua 3: Kujazia
Baada ya wiki 3, jazia na mbolea yenye nitrogen kama Mevuno Topdressing NPK 20.0.0. Katika wiki ya 5 kabla ya kutoa maua, ongezea tena na NPK 17:17:17 au 20:20:20. Unahitaji kilo 20/Ha.
Hatua 4: Kuweka miti
Funga mashina ya nyanya kwenye kamba kuimarisha mashina yasiyo imara. Hii
inahakikisha unapata matunda safi na yasiyo na magonjwa na kufanya uvunaji kuwa
rahisi.
Hatua 5: Kupogoa
Toa mashina yanayo chipuka pembeni kubaki na mashina yenye afya pekee.
Hatua 6: Malisho ya majani
Weka mbolea ya majani kwa uendanaji wa virutubisho sahihi vinavyohitajika na mmea wa nyanya katika hatua tofauti za ukuaji. Kwa mfano, nyunyizia EASY GRO flower and fruit NPK 14: 11:33 wakati wa kutoa maua kuboresha utoaji wa maua na kupunguza uharibikaji wa maua.