Wadudu na Magonjwa ya Nyanya
Wadudu
Kila mara kagua kuchunguza wadudu. Wadudu wa kawaida wanaoshambulia
mimea yako ya nyanya ni pamoja na:
Nziweupe
Ni wadudu wadogo weupe ambao hujificha chini ya majani. Wananyonya na kueneza magonjwa ya virusi katika mmea wako wa nyanya. Unaweza kutumia mitego yenye mnato au gamu kutoka Real IPM( +254 725 806086), Mtayarisho wa mwarubaini kama Nimbecidine au nyunyizia na viuadudu kama ASATAF.
Watoboa matawi (Leafminers)
Mdudu hatari sana anaekula majani, shina na matunda na kunyonya majimaji. Pia wanataga mayai kwenye majani ambayo hutotolea viwavi na kula majani. Utaona mistari mieupe kwenye majani. Matunda yataoza na shamba kukauka na kuonekana kama limechomeka na moto. Kukinga, tumia njia za kibailojia kama vile Diglyphus ambayo hula leafminer.
Wadudu wengine
- Vidakuri (Aphids):Utaona alama vyeupe juu ya majani.
- Siafi baibui wekundu: Ni wadudu wadogo ambao kufanya alama vyeupe- njano kwenye majani.
- Minyoo wa American Bull Worms na parare: Ni wadudu wanaotoboa majani.
Matatizo
Muozo wa ncha( Blossom end rot)
Hili ni tatizo la kawaida linalosababishwa na upungufu wa kalsiamu au kiwango kidogo cha Uchachu au pH katika udongo. Sehemu ya chini ya tunda hupata alama nyeusi na kuanza kuoza. Kudhibiti hili fanya kipimo cha udongo kujua afya ya udongo wako na Uchachu( pH ) kila miaka 2 -3.
Nyunyiza mbolea maji au foliar Spray iliyo na kalsiamu kama Easy Gro Calcium.
Magonjwa
Magonjwa mengi yanayovamia nyanya yanasababishwa na kuvu na bacteria. Haya ni pamoja na:
Kuchomeka kimapema na baadaye (Early and Late Blight)
Husababishwa na bacteria na kawaida katika msimu wa mvua. Majani na matunda yanaanza kutoa madoa meusi na kuanza kuoza. Kukinga: tumia mbegu zilizoidhinishwa/aina zinazohimili, fanya ubadilishaji wa mazao na zuia kwa viuatilifu kama Ridomil au Mistress kutoka Osho Chemicals.
Ukungu wa poda poda
Hufanya ukungu mweupe kwenye majani ambao hubadilisha majani kuwa njano na kukauka. Kuzuia, ondoa na angamiza mimea iliyoharibiwa na nyunyizia na viuatilifu kama Control 70DF
Kunyauka (Bacteria wilt)
Kunyauka haina tiba. Majani yatapukutika na yanaweza kukauka.
Muda wote tumia aina zinazohimili, fanya ubadilishaji wa mazao na tibu udongo
kabla ya kupanda. Ondoa mimea iliyoathiriwa.
Kunyauka ( Fusarium wilt)
Ni kuvu ya kawaida pia katika nyanya. Inapatikana kwenye udongo na kawaida katika msimu wa joto jingi. Dalili ni pamoja na kuwa njano na kunyauka kwa majani ya sehemu ya chini na kisha mmea wote kufa. Kukinga, panda aina zinazohimili na tibu udongo vyema kabla ya kupanda.
Kwa mengi kuhusu wadudu na magonjwa jiunge na iShamba au tuma SMS kwa 21606
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Nyanya
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure