Kuandaa Kitalu
    
    Hatua ya 1
Safisha magugu/kwekwe na nyasi zote. Lima udongo vyma mpaka kusiwe na madonge.
Hatua ya 2
Wiki 1 kabla ya kupanda, ongeza safu ya sentimita 7 ya mbolea ya samadi iliyooza vyema. Tumia toroli 1 uliojaa wa mbolea kwa kila mita 3 za mraba. Changanya kwenye udongo. Mwagilia (maji) tuta.
Hatua ya 3
Loweka mbegu kwenye maji baridi kwa masaa 24 kabla ya kupanda.
Hatua ya 4
Panda mbegu kwenye mistari sentimita 2 kwenda chini kwenye mishororo ya sentimita 15 kiumbali. Funika mbegu na safu nyepesi ya udongo. Ongeza nyasi kavu kama kivuli. Hii inalinda udongo na kuhifadhi unyevunyevu . Mwagilia (maji) matuta.
Uchipukaji
Mbegu zako zitaanza kuchipuza baada ya siku 5-7.Ondoa nyasi na weka kivuli juu ya kitalu.

- Kivuli kinatakiwa kuwa mita 1 juu.
Weka nyasi juu yake lakini hakikisha jua kiasi linaweza kupenya.
 - Ondoa miche dhaifu.Ipande kwenye tuta jingine.
 - Uweke udongo kuwa na unyevu unyevu. Maji mengi sana au kidongo sana ni mbaya kwa ya miche yako.
 
Maji mengi sana
- Virutubisho kwenye udongo vinaondolewa.
 - Kutakua na ukosefu wa hewa safi ya kutosha kwenye udongo.
 - Mmea utaanguka na shina litaoza.Mmea unaweza kufa.
 
Maji kidogo sana
- Mmea unanyauka.
 - Mmea hauwezi kuchukua virutubisho vyema hivyo ukuaji duni.
 
                        
                        
                        
                        
                        
                        
                