Kupandikiza miche yako

Pandikiza miche baada ya wiki 3-4. Pandikiza asubuhi mapema (saa 12-4 asubuhi) au jioni sana (saa 10-12 jioni)
Siku kabla ya kupandikiza, ondoa kivuli kwenye kitalu na punguza kumwagilia maji. Hii inaitwa mgandisho/imarisho. Inaipa miche nafasi ya kuzoea jua kali.
- Chimba mashimo ya kupandia sentimita 30 kiumbali kwenye mishororo ya sentimita 60 kiumbali.
- Changanya kifuniko cha chupa 1 cha TSP na kiganja cha mbolea ya samadi pamoja na udongo kwenye kila shimo.
- Panda miche.Mwagilia maji miche.
- Jazia na kijiko cha chakula 1 cha CAN kwa kila mmea wiki 3 baada ya kupandikiza.