Kuvuna

Kutegemea na aina ya spinachi, spinachi itakua tayari kwa kuvuna baada ya miezi 2-3. Katika hatua hii, itakua ishatoa/imezalisha majani makubwa, safi na yaliyokomaa.
Vuna majani mara mbili kwa wiki na tumia au peleka sokoni haraka iwezekanavyo. Utaendelea kuvuna kwenye miezi 2-3 inayofuata.
Kwa vile huharibika haraka,hakikisha kuna soko la tayari kabla ya kuvuna.