Sukuma wiki
Sukuma Wiki inajulikana sana kama Kale kwa Kingereza, ni zao la msimu mfupi ambalo linaweza kuoteshwa kwenye eneo ndogo.
Kabla haujaamua kupanda sukuma, unahitaji kuhakikisha kwamba udongo wako unafaa.Kujua hili,utahitaji kufanyia udongo kipimo/uchunguzi, ambacho kitakujulisha:
- Afya ya udongo wako
- Mbolea kiasi gani utahitaji kuongeza
- Mazao yatayakofanya vyema kwenye shamba lako.
Pigia CropNuts, huduma ya kupima udongo, Daktari Wa Udongo, kwenye +254 790 499190 au tuma barua pepe kwa support@cropnuts.com. Watachukua sampuli ya udongo wako kutoka shambani mwako na kukutumia majibu. Kipimo cha udongo kitaokoa pesa na kitakupa zao kubwa na bora.
Zinaota vyema kwenye hali ya baridi yenye nyizi joto 16-20℃, mvua iliyosambaa vizuri kwa 1500mm kwa mwaka na kati ya 800-200m.Hata hivyo kama upo kwenye eneo kame, unaweza kupanda sukuma kupitia umwagiliaji.
Udongo wenye maji na rotuba ya kutosha na viumbe hai na uchachu au pH wa kati ya 6-6.5, ni mzuri kwaajili ya sukuma wiki
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Sukuma wiki
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure