Kuandaa Kitalu

Nursery

Hatua ya 1

Ondoa magugu/kwekwe yote na nyasi. Lima udongo vizuri mpaka kusiwe na madonge

Hatua ya 2

Wiki 1 kabla ya kupanda, ongeza 7cm za mboji ama mbolea ya samadi iliyooza vyema.Tumia wheelbarrow 1 uliojaa mbolea ya samadi kwa kila mita 3 za mraba.Changanya kwenye udongo. Mwagilia maji tuta

Hatua ya 3

Loweka mbegu kwenye mchanganyiko wa PEARL gramu 50 ndani ya lita 20 za maji kabala tu ya kuzipanda. Hii itasaidia magonjwa yatokanayo na udongo kuvamia miche.

Hatua ya 4

Panda kwenye mistari ya sentimita 2 kwenda chini kwenye mishororo ya sentimita 15 kiumbali. Funika mbegu na tabaki jembamba la udongo. Weka  nyasi kavu kukufinaka . Hii italinda udongo na kuhifadhi maji. Mwagilia tuta. Weka udongo kuwa na unyevu nyevu lakini usitote.Maji mengi sana au kidogo sana ni mabaya kwa miche yako.

Kuchipuka

Mbegu zako zitaanza kuchipuka baada ya siku 5-7. Ondoa nyasi na weka kivuli juu ya kitalu.Spinach germination

Kivuli kiwe mita 1 juu. Weka nyasi kwa juu lakini hakikisha jua kiasi linweza kupenya.

  • Ondoa miche dhaifu.Ipande kwenye tuta jingine.
  • Weka udongo kuwa na unyevu nyevu lakini usitote. Maji mengi sana au kidogo sana ni mabaya kwa miche yako.

Maji mengi sana

  • Virutubisho kwenye udongo huoshwa.
  • Kutakua na upungufu wa hewa safi kwenye udongo.
  • Mmea utaanguka na shina litaoza. Mmea unaweza kufa.

Maji kidogo sana

  • Mmea hufifia.
  • Mmea hauwezi kuchukua virutubisho vizuri hivyo ukuaji duni.