Maandalizi ya shamba

Ploughing land preparation

Mara tu mbegu zinapopandwa kwenye kitalu chako, lima shamba lako. Vunja madonge ya udongo. Changanya mbolea ya samadi iliyooza vyema. Lainisha udongo.

Kipimo chako cha udongo kitakuambia mbolea gani za kuongeza kwenye udongo wako na kiasi gani. Kawaida utaambiwa kuongeza mbolea NPK wakati wa kupanda. Hii ina Naitrojeni, Fosfferi na Potasiamu, na mara nyingine na virutubisho vingine.

Mavuno Fertilizers (ARM Cement) wanatengeneza mbolea maalum kwaajili ya zao lako. Nunua mbolea za Mavuno kutoka kwa wauza pembejeo.

Magugu/Kwekwe

Magugu huchukua maji na virutubisho kutoka kwenye mmea wako. Pia huficha wadudu na magonjwa. Toa magugu unapoyaona.

Pia unaweza kutumia dawa za kuua magugu/kwekwe. Daima fuata maagizo na vaa nguo za kujikinga wakati unatumia viuakwewe.