Utamwagilia vipi maji mimea yako?

Drip irrigation

Maji ya kutosha ni muhimu kwa ukuaji wenye afya na kutoa mazao.Wakati mboga ina uhaba wa maji inaacha kukua na mara nyingi huanza kutoa mbegu kabla ya kukomaa(bolting) – au hata kufa.

Kwa afya, ukuaji imara na mavuno mengi, sukuma wiki yako inahitaji upatikanaji wa kila wakati wa maji kwenye mizizi. Lengo ni kufanya udongo na mboji kuwa nyevu nyevu muda wote.

Mbegu na miche ni hatua muhimu kwa mimea, hivyo hakikisha matuta ya miche na mbegu zilizopandwa zinakua na unyevu nyevu wakati wa mimea inakuwa.

Umwagiliaji wa tone kwa tone (Drip)

Umwagiliaji wa tone kwa tone unaweza kukusaidia kutumia maji kwa ufasaha. Mfumo wa umwagiliaji wa tone kwa tone au drip:

  • Unatumia maji kidogo kwani maji kutoka kwenye mifereji yanaenda moja kwa moja kwenye mizizi ya mmea. Maji hayapotei kwenye kwekwe.
  • Mimea haitoti maji.
  • Mara tu michirizi ya tone kwa tone inapowekwa,unatahitaji tu kufungua mfereji wakati unataka kumwagilia.

Kupata mfumo wa umwagiliaji wa tone kwa tone wa kwako, wapigie SunCulture kwenye +254 700 327 002. Pia unaweza kutembela tovuti yao kupata cheti cha bei.

Wakulima wa DLTP waliamua kununua pampu ya sola ya Futurepump kwa pamoja. Hii pampu inafanya kazi kwa kutumia nguvu kutoka kwenye jua.

Futurepump solar pumpUnaweza kulipia gharama za Futurepump baada ya misimu 3. Baada ya hapa, pampu yako haitaku gharimu!