Aina za Sukuma wiki

Thousand headed kale

Aina za kawaidia za Sukuma wiki ni pamoja na Marrow Stem, Thousand Headed, Sukuma Wiki Hybrid, Collard Southern Georgia na Collard Mfalme F1.

Wakulima wa DLTP waliamua kupanda aina ya Thousand Headed kutoka Royal Seed ambayo:

  • Ni refu sana, majani mengi na kuisha kwake hautambuliki. Hii inamaanisha unaweza kuvuna zaidi ya mara moja.
  • Hukomaa ndani ya siku 60 baada ya kuapanda.
  • Ina uhakika wa kuvuna tani 8( kilo 8000) kwa ekari.
  • Inastahimili vizuri sana joto.
  • Ina rangi ya kijani kibichi.

 Kwa matokeo mazuri haswa ukuaji na zao zuri, siku zote tumia mbegu zilizoidhinishwa.

Mbegu zilizoidhinishwa:

  • Hutoa mavuno mengi ya kiwango bora.
  • Hupunguza uwezekano wa zao kutomea.
  • Huhimili baadhi ya wadudu na magonjwa.
  • Hukua kwa haraka, imara na usawa.

Nunua mbegu zilizoidhinishwa kutoka kwa wauza pembejeo . Mbegu za Thousanda Headed huja kwenye pakti za gramu 10, gramu 25, gramu 50, gramu 100, gramu 250, na gramu 500.

Inashauriwa kuotesha miche yako kwenye kitalu au nunua kutoka kwa wakuza miche wenye sifa na kuaminika kama Plant Raisers.