Kupandikiza miche yako

Transplanting Kale

Pandikiza miche baada ya wiki 3-4. Pandikiza asubuhi mapema (saa 12-4 asubuhi) au jioni sana (saa 10-12 jioni).

Siku moja kabla ya kupandikiza,ondoa kivuli kwenye kitalu na punguza kumwagilia. Hii inaitwa Kuimarisha. Hutoa nafasi kwa miche kuzoea jua kali.

  • Chimba mashimo ya kupanda sentimita 30 kiumbali na mishororo sentimita 45 kiumbali.
  • Loweka udongo kwa mchanganyiko wa PEARL garmu 50 ndani ya lita 20 za maji kwenye knapsack. Hii itazuia magonjwa yatokanayo na udongo kuvamia miche. Loweka udongo kabla ya kuipanda.
  • Changanya kifuniko cha chupa 1 cha TSP na ujazo wa kiganya cha mbolea ya samadi na udongo kwenye kila shimo.
  • Panda miche. Mwagilia miche maji.
  • Jazia kwa CAN kijiko cha chai 1 kwa mmea wiki 3 baada ya kupandikiza.