Wadudu na Magonjwa ya Sukuma wiki

Spinach whiteflies

Wadudu

Whiteflies

Hawa ni wadudu wadogo wanaopatikana kwenye upande wa chini wa jani.Wananyonya utomvu kutoka kwenye mmea.

Kidukari

Kidukari ni mdudu mdogo wa kijani au njano anaepatikana kwenye majani ya mboga. Wananyonya utomvu kutoka kwenye mimea na pia kubeba magonjwa.

Magonjwa

Madoa kwenye majani/Leafspot

Spinach leaf spotHuu ni ugonjwa utokanao na udongo unaosababishwa na kuvu. Utaona madoa madogo ya kahawia kwenye majani na mwisho hufanya matundu kwenye majani.

Kudhibiti Leafspot, panda mbegu zilizoidhinishwa, badili mazao na tibu kutumia control au Sulcop kutoka Osho Chemicals.

Ukungu wa podapoda

Ukungu wa poda poda ni chipukizi jeupe la kuvu chini ya majani ambalo baadaye huzalisha madoa meusi au ya kahawia kwenye sehemu ya juu ya majani. Huanza mapema kwenye kitalu na kuendelea katika hatua zote za mmea, kama halijashughulikiwa vyema.

Kukinga, badili mazao kwenye shamba lako, fanya usafi mzuri kwenye kitalu chako na tibu kutumia Control au Mistress kutoka Osho Chemicals.