Kuandaa Kitalu
Hatua ya 1
Ondoa magugu/kwekwe yote na nyasi. Lima udongo vizuri mpaka kusiwe na madonge
Hatua ya 2
Wiki 1 kabla ya kupanda, ongeza 7cm za mboji ama mbolea ya samadi iliyooza vyema.Tumia wheelbarrow 1 uliojaa mbolea ya samadi kwa kila mita 3 za mraba.Changanya kwenye udongo. Mwagilia maji tuta
Hatua ya 3
Loweka mbegu kwenye mchanganyiko wa PEARL gramu 50 ndani ya lita 20 za maji kabala tu ya kuzipanda. Hii itasaidia magonjwa yatokanayo na udongo kuvamia miche.
Hatua ya 4
Panda kwenye mistari ya sentimita 2 kwenda chini kwenye mishororo ya sentimita 15 kiumbali. Funika mbegu na tabaki jembamba la udongo. Weka nyasi kavu kukufinaka . Hii italinda udongo na kuhifadhi maji. Mwagilia tuta. Weka udongo kuwa na unyevu nyevu lakini usitote.Maji mengi sana au kidogo sana ni mabaya kwa miche yako.
Kuchipuka
Mbegu zako zitaanza kuchipuka baada ya siku 5-7. Ondoa nyasi na weka kivuli juu ya kitalu.
Kivuli kiwe mita 1 juu. Weka nyasi kwa juu lakini hakikisha jua kiasi linweza kupenya.
- Ondoa miche dhaifu.Ipande kwenye
tuta jingine.
- Weka udongo kuwa na unyevu nyevu
lakini usitote. Maji mengi sana au kidogo sana ni mabaya kwa miche yako.
Maji mengi sana
- Virutubisho kwenye udongo huoshwa.
- Kutakua na upungufu wa hewa safi kwenye udongo.
- Mmea utaanguka na shina litaoza. Mmea unaweza kufa.
Maji kidogo sana
- Mmea hufifia.
- Mmea hauwezi kuchukua virutubisho vizuri hivyo ukuaji duni.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Sukuma wiki
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure