Kupandikiza miche yako

Pandikiza miche baada ya wiki 3-4. Pandikiza asubuhi mapema (saa 12-4 asubuhi) au jioni sana (saa 10-12 jioni).
Siku moja kabla ya kupandikiza,ondoa kivuli kwenye kitalu na punguza kumwagilia. Hii inaitwa Kuimarisha. Hutoa nafasi kwa miche kuzoea jua kali.
- Chimba mashimo ya kupanda sentimita 30 kiumbali na mishororo sentimita 45 kiumbali.
- Loweka udongo kwa mchanganyiko wa PEARL garmu 50 ndani ya lita 20 za maji kwenye knapsack. Hii itazuia magonjwa yatokanayo na udongo kuvamia miche. Loweka udongo kabla ya kuipanda.
- Changanya kifuniko cha chupa 1 cha TSP na ujazo wa kiganya cha mbolea ya samadi na udongo kwenye kila shimo.
- Panda miche. Mwagilia miche maji.
- Jazia kwa CAN kijiko cha chai 1 kwa mmea wiki 3 baada ya kupandikiza.