Wadudu na Magonjwa ya Sukuma wiki

Wadudu
Whiteflies
Hawa ni wadudu wadogo wanaopatikana kwenye upande wa chini wa jani.Wananyonya utomvu kutoka kwenye mmea.
Kidukari
Kidukari ni mdudu mdogo wa kijani au njano
anaepatikana kwenye majani ya mboga. Wananyonya utomvu kutoka kwenye mimea na
pia kubeba magonjwa.
Magonjwa
Madoa kwenye majani/Leafspot
Huu ni ugonjwa utokanao na
udongo unaosababishwa na kuvu. Utaona madoa madogo ya kahawia kwenye majani na
mwisho hufanya matundu kwenye majani.
Kudhibiti Leafspot, panda mbegu zilizoidhinishwa, badili mazao na tibu kutumia control au Sulcop kutoka Osho Chemicals.
Ukungu wa podapoda
Ukungu wa poda poda ni chipukizi jeupe la kuvu chini ya majani ambalo baadaye huzalisha madoa meusi au ya kahawia kwenye sehemu ya juu ya majani. Huanza mapema kwenye kitalu na kuendelea katika hatua zote za mmea, kama halijashughulikiwa vyema.
Kukinga, badili mazao kwenye shamba lako, fanya usafi mzuri kwenye kitalu chako na tibu kutumia Control au Mistress kutoka Osho Chemicals.