Kuhifadhi Viazi
Uhifadhi wa viazi pia nguzo muhimu ya kupata mavuno mengi. Kuhifadhi viazi vyako kuna faida nyingi nzuri.
Sio tu utazuia kupoteza kiasi flani cha mavuno yako kila mwaka kwa magonjwa, pia unaweza kuyaweka mpaka muda ambapo soko ni zuri.
Unda kikundi na majirani zako ili kuwauzia wanunuzi wakubwa. Ni rahisi kuuza magunia 1000 kuliko magunia 100. Utapata faida kubwa.
Hifadhi viazi vyako katika ghala la makaa
Njia nzuri ya kuhifadhi viazi vyako ni kutumia ghala linalopoozwa na mkaa
Jenga ghala kubwa la mkaa na majirani zako. Hifadhi mazao yako ya viazi mpaka miezi 3 -4.
Kuta za wazi zinatengenezwa na waya wa vyavu uliojazwa mkaa.
Mkaa muda wote huwekwa ukiwa na uvyevu kutoka kwenye tenki. Maji huwa mvuke kutoka kwenye mkaa inapo chukua joto kutoka ndani ya ghala. Hivyo ghala huwa na hali ya baridi sana. Pia lina giza – Hali mzuri sana kwaajili ya viazi!
Hakikisha magunia hayagusi kuta
Faida za ghala la mkaa
- Hakuna stima inayohitajika, ni maji tu.
- Linaweza kutumika kuhifadhia matunda totauti na mboga mboga.
- Huzuia matunda na mboga mboga kukauka
- Rahisi kujenga.
- Kama wakulima wengi wanajiunga pamoja kujenga ghala, sio ghali.
- Rahisi kudumisha.
Show times
Kenya
Sunday 1:30 pm (Swahili)
Thursday 1:30 pm (English)
Tanzania
Friday 6:30 pm (Swahili)
on ITV
Uganda
Sunday 3:30 pm (English)
on Urban TV
Viazi
Ushauri kwa matendo kuborsha shamba lako na kupata mavuno bora
Jisajili bure