Vitunguu

Sehemu nyingine na udongo ni nzuri kwaajili ya kupanda vitunguu kuliko kwengine. Kabla ya kufanya mipango zaidi, tambua kama vitunguu vitaota vyema kwenye shamba lako. 

Kabla haujaamua kupanda vitunguu, unahitaji kuhakikisha kwamba udongo wako unafaa. Kujua hili,utahitaji kufanyia udongo kipimo, ambacho kitakujulisha:

  •  Afya ya udongo wako
  • Mbolea kiasi gani utahitaji kuongeza
  • Mazao yatayakofanya vyema kwenye shamba lako.

Pigia CropNuts, huduma ya kupima udongo, Daktari Wa Udongo, kwenye +254 790 499190 au tuma barua pepe kwa support@cropnuts.com. Watachukua sampuli ya udongo wako kutoka shambani mwako na kukutumia majibu. Kipimo cha udongo kitaokoa pesa na kitakupa zao kubwa na bora 

Vitunguu huota vyema kwenye mwunuko chini ya  1,900m; mvua 500-700mm; joto kati ya 15­ - 30 ºC

Japo vitunguu vinaweza kuzalishwa katika aina nyingi za udongo, epuka udongo mzito kwani hii inaweza kupelekea matatizo kama uzungukaji wa hewa usiofaa, kupasuka na bidhaa zilizoharibika/kuparara yenye ubora wa kiwango cha chini.

Hakikisha kwamba udongo wako unatota vizuri angalau kina cha 60m. Undongo wa kina kifupi unaweza inaweza tumika, lakini  kuendane na vitendo vya usimamizi mahususi.

Jua zaidi kwa kubonyeza kwenye picha hapo chini.

Kwa wastani chuchu au pH mzuri ni 6.0 -6.8; viwango vya chini vya pH vinaweza kusababisha matatizo ya uchukuaji wa vijirutubisho.