Upandikizaji wa miche yako

Transplanting onion seedlings

Miche itakua tayari kwa kupandikiza baada ya wiki 4 ( siku 40, au wakati shina lina  unene sawa na penseli.

Hatua 1

Siku 7-10 kabla ya upandikizaji, taratibu punguza umwagiliaji na ondoa kivuli. Hii itaipa miche nafasi ya kuzoea mwangaza mkali wa jua

Hatua 2

Pandikiza asubuhi mapema ( 6-10am) au jioni (4-6pm).

Hatua 3

Masaa 2 kabla ya kupandikiza, mwagilia maji kitalu. Hili linakuwezesha kutoa kila mche na donge kidogo la udongo.

Hatua 4

Anza na miche imara na mizito. Unaweza kuacha miche isiyo imara kwenye kitalu kwa muda kidogo zaidi ili ziwe imara.

Hatua 5

Panda miche 10cm kutoka moja hadi lingine katika mishororo ya 30cm kati yazo. Panda kwenye mashimo yenye kina cha1.5cm na kisha imarisha miche na udongo unaozunguka.

Hatua 6

Kwekwe huchukua maji na virutubisho kutoka kwenye mimea. Pia huficha wadudu na magonjwa. Toa kwekwe wakati unapoyaona.Unaweza pia kutumia viuatilifu/viangamiza kwekwe. Daima fata maelezo na vaa nguo za kujikinga wakati unatupotumia viuatilifu.

Hatua 7

Jazia miche yako wakati vitunguu vyako vinakua vyema. Weka kilo 120 za CAN katika kila ekari. Nunua CAN kutoka kwa wakala wa kilimo.