Umwagiliaji wa mmea wako wa kitunguu

WateringUshawahi kuwaza namna utakavyomwagilia maji mimea yako?

Vitunguu vunahitaji maji kukua vyema. Hauwezi kutegemea mvua tu kwani muda mwingine hainyeshi. Mifereji , ndoo za kumwagilia maji, na vinyunyizi vya kumwagilia hupoteza muda na pesa.


Wakulima wa DLTP wameamua kuweka mfumo wa umwagiliaji wa drip kutoka SunCulture. Mfumo wa umwagiliaji wa drip:

Drip irrigation

  • Inatumia maji kidogo kwani maji kutoka kwenye mabomba huenda moja kwa moja kwenye mizizi ya mmea.
  • Maji hayapotezwi kwenye kwekwe.
  • Mimea haitoti.
  • Mara tu mistari ya drip inapowekwa, unatakiwa tu kufungulia mfereji pale unapohitaji kumwagilia.Wakulima wa DLTP pia waliamua kununua Futurepump pampu ya sola kwa pampoja. Waliokoa pesa nyingi za stima/umeme.

Futurepump solar pump

Pampu inafanya kazi kwa kutumia nguvu kutoka kwenye jua. Unaweza pia kuchaji simu yako kwaajili ya huduma za mabenki kwenye simu yako

Unaweza kulipa gharama za Futurepump baada ya misimu 3. Baada ya hapo, pampu yakoni bure!

Kwa taarifa zaidi, jiunge na huduma zetu za simu iShamba au kwa Kutuma Neno ‘VIJANA’ kwenda 21606.