Nini unatakiwa kufanya ukishindwa kulipa mkopo wako

Loan restructuring

Kuna hatua unaweza kuchukua kuhakikisha hili halitokei na unalindwa.

  • Kama unahisi utakosa rejesho la mkopo wako,ongea na mkopeshaji wako mara tu unapogundua hili.
  • Kama unahisi hali hii ni kwa muda mfupi, basi mkopeshaji wako atarekebisha mkopo wako ili kukuwezesha kuendana na nafikia marejesho yako.
  • Kama unahisi hii itakua hali ya muda mrefu kwa mfano,umepoteza mazao yako mengi kutokana na hali ya hewa mbaya au hali nyingine,basi unaweza kumuomba mkopeshaji wako mapumziko wakati unashughulikia jinsi utakavyolipa deni hili.Kawaida mkopeshaji atahitaji mpango wa kujikwamua kutoka hali yako na anaweza akateua afisa mkopo wa kukusaidia kuandaa mpango wa kurejesha.
  • Unaweza kufikiria kuipa kipaumbele mikopo yako.Kuna baadhi ya mikopo ambayo inaweza kuwa haina haraka sana kuliko mingine na unaweza kutumia pesa iliyokusudiwa kulipia mikopo kama hii kulipa mikopo yenye uharaka zaidi kama mkopo wa benki.