Vitu vya kuzingatia wakati wa kuchukua mkopo

Loan_Things to consider

Kuna vitu vingi vya kuzingatia wakati wa kuchukua mkopo:

  • Kiasi gani unachohitaji?
  • Utalipaje mkopo? Una kipato cha uhakika?Una kumbukumbu za kuambatanisha na hili?
  • Taasisi ya kifedha ni ya kuaminika? Sifa zake ni zipi?
  • Taasisi ya kifedha ina bidhaa/sera maalum za mkopo zinazoendana na mahitaji yako, k.m sera kwaajili ya wanawake, vijana, wakulima na kadhalika?
  • Kama unapata kipato kwa msimu, je ulipaji wa mkopo wako unaweza kupangwa kulingana na hili?
  • Riba ni ya kiasi gani?
  • Gharama gani zingine zilizopo zilizojificha?
  • Ni dhamana gani ya mkopo taasisi ya kifedha inahitaji? Dhamana ni kitu chenye thamani ambacho unamiliki kama vile gari au hati ya kiwanja/nyumba ambayo benki inaweza kuchukua kama utashindwa kulipa mkopo.
  • Je unaweza kutumia simu yako ya mkononi kulipia mkopo?
  • Kuna gharama utatozwa kama utalipa mkopo wako kimapema kabla ya muda wa kulipa?
  • Je malipo ya mkopo wako  yanaweza kucheleweshwa kama hutaweza kulipa kuendana na muda wake?
  • Je taasisi ya kifedha itakuadhibu kama hutalipa mkopo wako kwa wakati?