Kuelewa viwango vya riba

Interest rates

Wakati unakopa pesa kutoka kwa taasisi za kifedha zilizo rasmi, makundi ya Akiba na mkopo/SACCOS na hata taasisi za kifedha zisizo rasmi, kiasi unachotakiwa kulipa daima kitajumlisha kiwango cha riba na gharama zingine zozote za ziada au ada.

Kiwango cha riba ni gharama ya kukopesha pesa. Hii kwa kawaida ni asilimia ya thamani kwa mwaka au mwezi. Unapolipa pesa uliyokopa, utalipa kiasi asilia jumlisha kiwango cha riba.

Kiwango cha riba kinaweza kuwa tofauti kama unakopa pesa kwa muda mfupi kuliko wakati unakopa pesa kwa muda mrefu.Kiwango cha riba pia kinaweza kupanda au kushuka wakati wowote kutokana na mfumuko wa bei, nguvu za soko na hata sharia za benki kuu.