Nini kinatokea usipolipa mkopo wako?

Kuna vitu vingi vinaweza kutokea wakati usipoheshimu mkataba wa marejesho yako ya mkopo:
- Utalipishwa ada au riba ya ziada na kuongezewa kwenye mkopo wako.
- Unaweza kushtakiwa kwa Mamlaka ya Dhamana ya Mkopo( Credit Reference Bureau)
- Mkopeshaji wako anaweza kuwaambia wakusanyaji wa madeni kujaribu na kupata unachodaiwa kutoka kwako.Kwenye hili wakulima wengi wameripoti mifugo na hata mashamba yao kuchukuliwa na benki na wakopeshaji wengine.
- Unaweza kushtakiwa mahakamani ambapo unalazimishwa kulipa mkopo wako au kutumikia kifungo jela.
- Unahatarisha kupoteza dhamana yako.
- Kama ulikua na wadhamini wa mkopo, wanaweza kulazimishwa kulipa mkopo huo kwa niaba yako.
- Unaweza kuwa na wakati mgumu kupata mkopo mwingine huko mbeleni/sikuzijazo