Fanya utafiti

- Siku zote unatakiwa kusoma nyaraka zako za mkopo kwa umakini kabla ya kuweka sahihi kwaajili ya mkopo.Daima uliza kama kuna ada ya nyongeza.
- Siku zote unaweza kumuuliza mkopeshaji wako akuambie kiasi utakachohitajika kulipa kwa thamani halisi kuliko asilimia, kufanya rahisi kwako kuelewa nini unadaiwa.
- Fanya utafiti na ulinganishe riba za taasisi tofauti za kifedha, ili uweze kupata mkopeshaji unaemudu na anaendana na mahitaji yako.
- Hakikisha mkopeshaji wako ni wa kuaminika.Uliza maswali mengi uwezavyo ili kufanya maamuzi yako. Kama mkopeshaji hayuko tayari kujibu maswali yako, basi huyo sio mkopeshaji sahihi kwaajili yako.