Kujenga alama yako ya mkopo

Alama yako ya mkopo ni nambari ambayo inaonyesha jinsi unavyomudu fedha na inamfanya mkopeshaji kujua kama wewe ni mkopeshwaji mzuri au sio na utaweza kurudisha kile wanachokukopesha. Alama nzuri ya mkopo ina maanisha mkopeshaji ataridhia na kuwa nautulivu hata akikupa kiasi kikubwa cha fedha
Unaweza kujenga hizi alama kwa:
- Siku zote kuheshimu mikataba ya marejesho ya mkopo wako ulionao kwa wakati.
- Unaweza kuanza kwa kuchukua mikopo midogo( mfano mkopo wa simu kama Mshwari na KCB M-PESA) na kuilipa kwa wakati. Mikipo mingi unavyochukua na kulipa kwa wakati, ndio unakuongezea alama zako.