Vitu vya kuzingatia wakati wa kuchukua mkopo

Kuna vitu vingi vya kuzingatia wakati wa kuchukua mkopo:
- Kiasi gani unachohitaji?
- Utalipaje mkopo? Una kipato cha uhakika?Una kumbukumbu za kuambatanisha na hili?
- Taasisi ya kifedha ni ya kuaminika? Sifa zake ni zipi?
- Taasisi ya kifedha ina bidhaa/sera maalum za mkopo zinazoendana na mahitaji yako, k.m sera kwaajili ya wanawake, vijana, wakulima na kadhalika?
- Kama unapata kipato kwa msimu, je ulipaji wa mkopo wako unaweza kupangwa kulingana na hili?
- Riba ni ya kiasi gani?
- Gharama gani zingine zilizopo zilizojificha?
- Ni dhamana gani ya mkopo taasisi ya kifedha inahitaji? Dhamana ni kitu chenye thamani ambacho unamiliki kama vile gari au hati ya kiwanja/nyumba ambayo benki inaweza kuchukua kama utashindwa kulipa mkopo.
- Je unaweza kutumia simu yako ya mkononi kulipia mkopo?
- Kuna gharama utatozwa kama utalipa mkopo wako kimapema kabla ya muda wa kulipa?
- Je malipo ya mkopo wako yanaweza kucheleweshwa kama hutaweza kulipa kuendana na muda wake?
- Je taasisi ya kifedha itakuadhibu kama hutalipa mkopo wako kwa wakati?